Kiungo wa Liverpool, Naby Keita atajiunga na timu ya Bundesliga ya Werder Bremen wakati mkataba wake utakapomalizika na klabu hiyo ya Anfield katika kipindi cha majira ya joto.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye amefunga mabao 11 katika mechi 129 kwa Liverpool, alisaini kwa kile kinachoitwa rekodi ya klabu ya Pauni milioni 48 kutoka RB Leipzig mwaka 2018.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Guinea amecheza mechi nane za ligi msimu huu kutokana na majeraha.

Hata hivyo Klabu ya Liverpool tangu Mei ilithibitisha kuondoka kwake.

Keita amefanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa, Kombe la Dunia la klabu, Kombe la FA na EFL katika kipindi chake cha miaka mitano alichokuwa England.

“Klabu kadhaa ni wazi zitakuwa zinamtaka wakati anapokuwepo mchezaji kama Keita, “amesema Clemens Fritz, kiongozi wa kusaka vipaji na soka la kulipwa katika klabu ya Werder Bremen.

“Amekuwa akikabiliwa na maumivu mwanzoni mwa msimu huu na hiyo ina maana kuwa hakucheza mara nyigi kama alivyokuwa akitaka. “Sasa tunataka kumrudisha katika kuwango chake bora.”

Young Africans waipa kongole Azam FC
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 12, 2023