Beki wa Real Madrid, Nacho Fernandez amefunguka kawa, atasaini mkataba na kuendelea kuwa ndani ya viunga vya Santiago Bernabeu mpaka msimu ujao 2023/24.
Nacho anatarajiwa kuiongoza Real Madrid kama nahodha msimu ujao baada ya Karim Benzema kuondoka kikosini hapo.
Beki huyo mkataba wake na Madrid ulikuwa unamalizika Juni 30, mwaka huu, lakini amekubali kuongeza mwaka mmoja kusalia kikosini hapo.
Dili lake jipya la kuendelea kusalia ndani ya Madrid anatarajiwa kusaini hivi karibuni.
Nacho ni kati ya wachezaji wakongwe ambao wamesalia ndani ya Real Madrid akiwa sambamba na Luka Modric na Toni Kroos.
Beki Huyo alisema:. “Nimeamua kubaki Madrid Real, ni kweli nilikuwa na ofa nyingi lakini pia nilitaka kubaki hapa, hivyo nina furaha kuendelea kusalia hapa tena kwa mwaka mwingine.”
Ikumbukwe katika msimu uliomalizika wa 2022-23, Nacho hakutumika sana katika kikosi cha kocha Carlo Ancelotti.