Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi ( NACTE) limetoa ufafanuzi kuhusu malalamiko ya kuchelewa kupata Namba ya Uhakiki wa Tuzo (AVN) yanayotolewa na baadhi ya wahitimu wa ngazi ya stashahada hasa waliomaliza masomo katika mwaka wa masomo wa 2017/18.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mkuu wa Kitengo cha Udahili NACTE, Twaha A. Twaha, wakati akizungumza na waandishi habari ambapo amesema kuwa kitendo cha vyuo na taasisi za elimu kutowasilisha mapema matokeo halisi ya wahitimu kwenye baraza hilo, kimepelekea wahitimu hao kukwama katika maombi ya AVN.

Amesema kuwa hakuna mhitimu wa ngazi ya diploma anayeweza kujiunga na elimu ya juu bila ya kuwa na AVN na kwamba wahitimu hao wanapaswa kuwa na vigezo stahiki wakati wanapofanya maombi NACTE ili wapate namba hiyo itakayowawezesha kujiunga na vyuo vya elimu ya juu.

“Kumekuwepo na malalamiko ya baadhi ya wahitimu wa ngazi ya stashahada na hasa waliomaliza masomo yao kwa mwaka wa masomo 2017/2018 hadi mwezi Julai, 2018. baadhi ya wahitimu hao mara tu baada ya kumaliza mitihani yao na kupatiwa matokeo ya awali wamekuwa wakiomba AVN kwa kuambatanisha hati za matokeo ya awali wakati vyuo na taasisi husika hazijawasilisha NAVTE matokeo halisi yaliyoidhinishwa na mamlaka husika,” amesema Twaha na kuongeza.

Hata hivyo, kufuatia malalamiko hayo, Twaha amevitaka vyuo na taasisi za elimu kutoa matokeo ya wahitimu wao mapema kwa ajili ya kuwarahisishia kupata Namba ya Uhakiki wa Tuzo (AVN) itakayowawezesha  kujiunga na elimu ya juu

Barabara ya chini ya Ardhi ya kusafirisha dawa za kulevya yagundulika
Ruto ajibu utafiti unaoonesha anatajwa kuongoza kwa rushwa