Endapo marekebisho ya Sheria ya Ardhi yaliyopendekezwa Bungeni yatapita, yatasadia kupunguza gharama za upangaji, urasimishaji na umilikishaji wa ardhi nchini, ili kuziwezesha Halmashauri nchini kufuatilia ukusanyaji wa kodi ya Pango.

Akizungumza hii leo Bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchema amesema mapendekezo hayo ni pamoja na kupunguza tozo ya malipo ya mbele (Premium), kutoka asilimia 0.5 ya thamani ya ardhi hadi asilimia 0.25.

Amesema, mengine ni kupunguza ada ya hati miliki kutoka shilingi 50,000 kwa hati hadi shilingi 25,000
kwa hati, kupunguza ada ya usajili wa hati kutoka asilimia 20 hadi asilimia 10 na kupunguza ada ya maombi ya hati kutoka shilingi 20,000 hadi shilingi 5,000.

“Mheshimiwa Spika, pia napendekeza kufuta ada ya mpango wa upimaji (Deed Plan) ambayo ilikua inatozwa shilingi 20,000 na kurekebisha Sheria ya Ardhi, Sura 113 ili Mkurugenzi wa Halmashauri akasimiwe jukumu la kukusanya Kodi kwa niaba ya Wizara ya Ardhi,” amesema Waziri huyo.

Aidha, ameongeza kuwa asilimia 20 ya mapato hayo yatarejeshwa yatarejeshwa Halmashauri ili kuziwezesha katika ufuatiliaji na ukusanyaji wa kodi hizo, hatua ambazo zinatarajia kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 115,500.

Marekebisho ya sheria kufuta tozo miamala ya Simu
Tozo juu Michezo ya kubahatisha