Nahodha wa Meli iliyokuwa imebeba takriban watu 400, kupoteza mwelekeo na kujaa maji ikiwa katika meneo ya kati ya Ugiriki na kisiwa cha Malta amekimbia kusikojulikana huku ongezeko kubwa la boti zilizobeba wahamiaji zikivuka bahari ya Mediterania kutokea Afrika Kaskazini.

Shirika lisilo la kiserikali la Ujerumani, Sea-Watch International limesema limeipata boti hiyo ikiwa jirani na meli mbili za wafanyabiashara na mamlaka ya Malta iliziamuru meli hizo kutofanya uokoaji na kwamba moja kati ya meli hizo iliombwa kuijaza mafuta.

Manusura wa Mashua ya wahamiaji iliyopinduka wakiwa jirani na kisiwa cha New Providence, Bahamas. Picha na Kitini / Jeshi la Ulinzi la Royal Bahamas / AFP.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, pia walipokea simu kutoka kwenye boti hiyo iliyosafiri usiku kucha ikitokea katika jiji la Tobruk, nchini Libya na kuziarifu mamlaka ingawa haijaanzisha operesheni ya uokoaji mpaka sasa.

Huduma hiyo ya simu, ilisema boti hiyo kwa sasa iko katika eneo la Uokoaji na Utafutaji (SAR) katika kisiwa cha Malta. Alarm Phone imesema watu waliokuwemo kwenye meli hiyo walikuwa katika taharuki, ambapo wengi wao wakihitaji matibabu.

Sababu za Ushindi wa Mil 26 Zatajwa na Muhusika
Marcus Rashford hali tete Man Utd