Nahodha wa kikosi cha Geita Gold FC, Jofrey Manyasi ameunguruma kwa mara ya kwanza jijini Dar es salaam, akizungumzia Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya klabu yake kupanda daraja ikitokea Ligi Daraja la Kwanza.

Manyasi ameunguruma mbele ya waandishi wa habari katika mkutano maalum uliokua na lengo la kuzungumzia maandalizi ya kikosi chao kuelekea mchezo wa mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu dhidi ya Young Africans kesho Jumamosi (Oktoba 02), Uwanja wa Benjamin mkapa jijini Dar es salaam.

Manyasi amesema:”Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Yanga na tunaamini kwamba tutapata ushindi na tumejiandaa.”

“Wachezaji tunajua kwamba tumetoka kupoteza pointi mbele ya Namungo FC hivyo tuna kazi ya kufanya mashabiki wajitokeze kwa wingi.”

Geita Gold FC inayonolewa na Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Etienne Ndayiragije akisaidiwa na Fred Felix Minziro, ilipoteza mchezo wa mzunguuko wa kwanza dhidi ya Namungo FC kwa kufungwa mabao 2-0, Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.

Ufafanuzi kutoka kwa Peter Banda
Minziro: Geita itapambana, hatuiogopi Young Africans