Nahodha wa timu ya taifa, Nadir Haroub au maarufu kama Canavaro amesema kuwa atastaafu kuichezea timu hiyo baada ya miaka mitatu, licha ya kuzua gumzo kuwa kiwango chake kimeshu…

kwa mujibu wa habari iliyoandikwa na gazeti la  Habari Leo, ‘Canavaro’, ambaye pia ni beki wa Yanga alisema maneno ya kejeli hayawezi kumvunja moyo na kutangaza kuachana na soka ili hali umri wake si mkubwa kiasi cha kushindwa kuhimili mikikimikiki ya dakika 90 uwanjani.

“Hizi kejeli na maneno ya watu nimeyazoea muda mrefu kuhusu kiwango changu kushuka au umri kuwa mkubwa, hivyo nimeamua kunyamaza tu”, alisema Canavaro.

“Muda wa kustaafu haujafika, nafikiria kufanya hivyo baada ya miaka mitatu na nikistaafu bado nitaendelea na kuichezea Yanga, na ikitokea nimeondoka Yanga basi ndio mwisho wa jina langu kusikika kwenye soka, kwani sifikirii kuichezea timu nyingine baada ya hapo,” alisema Canavaro Baada ya timu ya Taifa ya Tanzania kuondolewa kwenye mbio za kuwania kucheza Kombe la Dunia 2018 na Algeria baada ya kufungwa mabao 7-0 kwenye mchezo wa marudiano nchini Algeria, kuliibuka maneno kuwa Canavaro na beki mwenzake Kelvin Yondani wameshuka viwango vyao kutokana na umri wao kuwa mkubwa.

Taifa Stars iliondolewa baada ya kufungwa jumla ya mabao 9-2 kufuatia sare ya 2-2 kwenye Uwanja wa Taifa na kipigo cha mabao 7-0 nchini Algeria katika mchezo wa marudiano. Kwa mujibu wa taarifa za mtandaoni, Cannavaro alizaliwa Februari 10, 1982 na sasa ana umri wa miaka 33.

Marinica: Tunaweza Kuifunga Timu Yoyote Ligi Kuu
Van Gaal Atoa Nasaha Nzito Kwa Wachezaji Wa United