Naibu Kamishna wa Polisi, Dhahiri Kidavashari amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo Jijini Dodoma wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya Christian Medical Center Trust (DCMCT) iliyopo Ntyuka, Dodoma ambako alikuwa akipatiwa matibabu..

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, Kamanda Dhahiri Kidavashari, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Novemba, 17, 2020 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

Aidha IGP Sirro, amesema kuwa msiba upo Kisasa, Nyumba mia tatu jijini hapo huku taratibu za mazishi zikiwa zinaendelea.

Msemaji wa Polisi, David Misime amesema, Kamanda Kidavashari alilazwa tangu Novemba 15 na ataagwa kesho, kisha mwili wake utasafirishwa kwenda mkoani Arusha kwa ajili ya maziko.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 18, 2020
Watanzania watatu washikiliwa Kenya