Naibu Waziri wa Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Longido Mkoa wa Arusha Dkt Steven Kiruswa ametoa agizo kwa mmiliki wa Mgodi wa PARAMOUNT LTD unaofanya shughuli za Uchimbaji katika Kijiji Cha Sinoniki na Kimwati katika tarafa ya Engarenaibor huko wilayani Longido kuhakikisha anafuata taratibu za upataji wa eneo la Ardhi kwa kupitisha kwenye mkutano Mkuu wa Kijiji.
” Nimeona hapa Kimwati mmefuata utaratibu wote unaotakiwa,lakini Sinoniki hamjafuata taratibu naomba mkaliweke sawa kabla wizara haijachukua hatua Kali za kisheria lakini pia mkifuata taratibu mtaepuka migogoro na jamii” alisema Dkt Kiruswa.
Dkt Kiruswa amewataka kufuata taratibu zote za kisheria ili kuepuka migogoro na jamii ikiwemo masuala ya uhifadhi wa mazingira pamoja na kuweka makubaliano yenye kuonekana kwa jamii ikiwemo kusaidia miradi ya Maendeleo.
“Nakuagiza Mwenyekiti wa Kijiji kaitisheni kikao Cha serikali ya Kijiji hata Cha dharau ,na ifikapo wiki ijayo taarifa ya makubaliano hayo yawe yamefika kwa Mkuu wa Wilaya Longido na sisi wizarani tutapata na kuangalia Kama yapo sawa” alisema Dkt Kiruswa.
Hata hivyo amewashauri wawekezaji hao kufanya utafiti zaidi(Exploration) kabla ya kuanza Uchimbaji au kuendelea kufanya Uchimbaji kwa kukisia pasipo kuwa na uhakika pomoja na kuweka utaratibu wa kusoma taarifa za miradi waliyoitekeleza kwa jamii katika mikutano mikuu ya vijiji.
Katika hatua nyingine pia amewataka kutumia utaalamu wa kuchimba Madini aina ya Vito