Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, ameitaka jamii kutoa ushirikiano hasa katika kusaidia watoto wenye uhitaji maalumu ili watoto wote waweze kupata msaada na kutimiza ndoto zao.
Amesema hayo wakati akizungumza na Dar24 Media katika mashindano ya MOI Marathoni lengo likiwa ni kusaidia watoto takribani 40 wenye kibiongo ambapo mtoto mmoja ni milioni nne ambapo marathoni hiyo ilikuwa inatafuta zaidi ya milioni 160 .
”Niwashukuru sana kwa kijitokeza kwa wingi kwasababu kwa sasa sawa mipango ni kuwatafutia fedha hawa watoto 40 lakini watoto wenye uhitaji wapo wengo kwahiyo tulitamani watoto wote wenye uhitaji wapata huduma kwahiyo hata marathoni hii ikiisha watu waendelee kutoa michango” amesema Dkt. Tulia