Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Clement Kivegalo kufanya mabadiliko ya wataalamu katika wilaya hiyo amabpo ameagiza kumuondoa meneja wa Wilaya ya Mbarali (RUWASA), Job Mwakasala.

Naibu Waziri amechukua uamuzi huo kufuatia kutoridhishwa na utendaji kazi wao baada ya kukuta changamoto nyingi katika wilaya ya Mbarali huku wakishindwa kuchukua hatua sahihi kuzitatua.

Mhandisi Mahundi amesema wananchi wa wilaya ya Mbarali wana kero nyingi kuhusiana na huduma ya maji huku wasimamizi wakishindwa kuwahudumia badala yake wakitoa taarifa zilizo tofauti ukilinganisha na uhalisia wa hali iliyopo, jambo linalokwamisha jitihada za serikali kutatua kero za wananchi.

 Hata hivyo Naibu Waziri Maryprisca ametangaza kuivunja Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Mji Mdogo wa Rujewa katika wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya kwa kushindwa kuisimamia ipasavyo menejimenti ya mamlaka hiyo.

Azam FC yawakana Chikwende, Mgore
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 4, 2021.