Waziri Mkuu nchini Uingereza, Thereasa May amemfukuza kaziĀ  Naibu wake Waziri Damian Green, mara baada ya kukutwa na picha za ngono kwenye kompyuta yake ya ofisini na kushindwa kutoa taarifa zilizo sahihi kuhusu picha hizo.

Ambapo uchunguzi kwenye ofisi ya baraza la Mawaziri umesema, Waziri Green alitoa taarifa ambazo hazina ukweli zilizopotosha akikataa kuhusika na video hizo.

Kupitia tukio hilo, na tuhuma zinazomkabili, Green alilazimishwa na washauri wake kuandika barua ya kujiuzulu kwani amevunja maadili ya uwaziri.

Tofauti na kosa hilo Waziri huyo Damian Green alikuwa anachunguzwa pia juu ya madai ya kutowaheshimu wanawake wanaharakati ambao wako katika chama chake cha Conservative.

Green alikuwa mshirika mkubwa wa waziri mkuu, na kuondoka kwake kutakuwa ni pigo kubwa kipindi hiki ambacho Uingereza inapitia kwenye majadiliano ya kujitoa Umoja wa Ulaya.

 

Marion Bartoli atengua maamuzi
Heche: Takwimu zinazotolewa na serikali si sahihi