Namelock Sokoine, mtoto wa waziri mkuu wa zamani, Edward Sokoine amepewa nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Edward Lowassa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Monduli.

Namelock ambaye amekuwa akikiri kuwa alilelewa kisiasa na Lowassa, amepita bila kupingwa kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), akiwakilisha wilaya hiyo. Nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Edward Lowassa kabla ya kuhamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kugombea urais.

Ushindi wa Namelock ulitangazwa jana na Katibu Mkuu wa Chama hicho wilaya ya Monduli, Elisante Kimaro ambaye alieleza kuwa Namelock alipita bila kupingwa baada ya mpinzani wake, Nyanoni Ole Supuku kushindwa kutorejesha fomu.

Namelock aligombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM lakini alishindwa na mgombea wa Chadema, Julius Kalanga.

Dylan Kerr: Siondoki Dar es salaam Mpaka Nilipwe Changu
Mahakama yatoa uamuzi kesi ya Uchaguzi wa Umeya, Ilala na Kinondoni