Mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya Mjini Sugu, Faiza Ally amesema amependezwa na tukio la kufunga ndoa kwa, Joseph Mbilinyi amesema kuwa anaamini sasa Mbunge huyo anaenda kuwa na maisha ya furaha zaidi.

Faiza ametoa kauli hiyo ikiwa ni muda mchache baada ya Mbunge Sugu kufunga ndoa na mkewe Happines Msonga, ambapo kupitia mtandao wake wa Instagram, amesema licha ya Sugu kuoa bado ana mapenzi na yeye.

“Kuna mtu anayenipenda sana alinipa ratiba nzima mwezi mmoja kabla ya ndoa na kabla ya hapo nilijua kama wataoana ila siku ya tukio ni siku ya tofauti, hata mwanzoni nilipotaka kufanya jambo nilijikuta nakosa hisia za kufanya kwa sababu sina tena majonzi juu ya baba Sasha,”amesema Faiza.

Ameendelea kusema, “nikimwangalia baba Sasha na mke wake sioni mtu wa kuniliza na najiuliza nilikosea wapi, kwa sababu nilikuwa mpenzi bora, nilikuwa mama bora kwahiyo sijapata mwanaume tu wa kunielewa mimi. Anaoa lakini najua bado ananipenda mimi”.

Mapema jana Agosti 31, 2019 Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Mr.II Sugu’ alifunga ndoa na mpenzi wake Happiness Msonga, katika kanisa Katoliki, Ruanda jijini Mbeya.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Septemba 2, 2019
Tanzania imeamua kutekeleza miradi ya maendeleo- Msemaji wa Serikali