Wakati kikosi cha timu ya Namungo kikirejea salama Jijini Dar es Salaam tayari kwa maandalizi ya mchezo ujao dhidi ya Pyramid ya Misri Machi 17 katika dimba la Azam Complex Chamazi,  wachezaji wao wamepewa saa 20 za mapumziko.

Namungo wamerejea saa 12:00 asubuhi leo Ijumaa (Machi 12) wakitokea Nchini Morocco ambapo Jumatano (Machi 10) walikuwa na kibarua cha kuwakabili Raja Casablanca katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi huku wachezaji wakiruhusiwa kwenda nyumbani kwao saa 5:00 asubuhi mpaka kesho saa 3:00 asubuhi.

Mkuu wa Idara ya Habari ya Klabu hiyo Kindamba Namlia amesema, kikosi chao kimerejea salama Jijini Dar es Salaam na kwenda moja kwa moja kambini, na muda mchache Kocha wao Mkuu Hemed Morocco amewaruhusu kwenda majumbani na kurejea kesho.

Namlia amesema kwa sasa wameitupia kisogo Raja Casablanca kwa kuwa ni mchezo ambao tayari umepita wanatizama mbele zaidi waweze kufanya vizuri katika mchezo ujao dhidi ya Pyramids.

Namungo FC inashiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza, baada ya kushika nafasi ya pili kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho nchini Tanzania ‘ASFC’ nyuma ya Simba SC msimu wa 2018/20.

Taifa Stars kuifuata ‘Harambee Stars’ kesho
Majaliwa azungumzia hali ya Rais Magufuli