Imefahamika kuwa wawakiilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika Namungo FC itawekwa kwenye chungu cha nne, wakati wa upangaji wa makundi ya michuano hiyo baadae leo hii mjini Cairo, Misri.
Namungo FC tayari inaongoza kwa mabao sita kwa mawili dhidi ya Clube Desportivo 1º de Agosto ya Angola, huku ikisubiri mchezo wa mkondo wa pili ambao utachezwa juma hili.
Mshindi wa jumla wa mchezo huo ambaoutachezwa nchini Tanzania ataingia moja kwa moja kwenye hatua ya makundi, na tayari Namungo FC wametanguliza mguu moja kwenye hatua hiyo.
Michezo mingine ya hatua ya 32 ya michuano hiyo imeshakamilika na timu zimeshapangwa kwenye vyungu ambavyo vitatumika kupanga makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Chungu cha Kwanza: RS Berkane, Etoile Sahel, Raja Club Atl na Enyimba FC
Chungu cha Pili: Pyramids FC, CS Sfaxien, ES Setif na JS Kabylie
Chungu cha Tatu: Orlando Pirates, Salitas FC, Cotonsport, Nkana FC
Chungu cha Nne: ASC Jaraaf, Al Ahli Benghazi, NAPSA Stars na Namungo SC *