Baada ya kuwasili nchini Jana Jumatatu (Februari 15) wakitokea Angola alipokua wamekwama kwa siku tatu, Uongozi wa klabu ya Namungo FC umeweka wazi kadhia zilizowakuta walipokua mjini Luanda.

Namungo FC ilisafiri hadi mjini humo mwishoni mwa juma lililopita kwa ajili ya mchezo wa hatua ya 32 bora dhidi ya 1 de Agosto ya Angola ambayo ni mali ya Wanajeshi.

Mchezo huo ambao ulipangwa kuchezwa Februari 14 ulifutwa na Shirikisho la Soka Afrika, ‘CAF’ kutokana na wachezaji wa Namungo FC pamoja na viongozi kutakiwa kukaa karantini kwa muda kabla ya mchezo.

Mwenyekiti wa klabu hiyo yenye maskani yake kusini mwa Tanzania Hassan Zidadu, amesema hawana furaha kwa kile walichofanyiwa kwa kuwa walinyanyaswa bila hatia, tena wakiwa ugenini.

“Tumenyanyaswa bila sababu kwa kuwa hakuna maelezo mazuri ambayo tulikuwa tunapewa, ndani ya mioyo yetu hatukuwa na amani kabisa na tunashukuru kwa dua za Watanzania.”

Hata hivyo wachezaji watatu na kiongozi mmoja wameendelea kuzuiwa nchini Angola kwa kile ambacho kilielezwa kuwa wamekutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona jambo ambalo limekuwa likipingwa na viongozi wa Namungo FC.

Mexime aichimba mkwara Young Africans
Ajabu: Mfahamu binadamu aliyeishi na watu 24 ndani ya mwili wake