Mshindi wa jumla wa mchezo wa hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Namungo FC ya Tanzania dhidi ya Clube Desportivo 1º de Agosto ya Angola.

Namungo FC tayari imeshaingia mguu mmoja kwenye hatua ya makundi baada ya kuifunga Clube Desportivo 1º de Agosto ya Angola mabao 6-2 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa jana jijini Dar es salaam.

Mchezo wa pili Namungo FC watakua ugenini ambapo watalazimika kulinda ushindi wao ili kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo ambayo inashiriki mchuano ya kimataifa kwa mara ya kwanza.

Namungo FC/ Clube Desportivo 1º de Agosto imepangwa kundi D na wakongwe na wazoefu katika michuano ya kimataifa kama Raja CA, Pyramids FC na Nkana FC.

Fenerbahce kumuweka sokoni Samatta
Masau Bwire amlaumu Martin Saanya

Comments

comments