Klabu ya Namungo imefikia makubaliano ya kunasa saini ya mshambuliaji, Kelvin Sabato kwa mkataba wa miaka miwili.

Sabato amejiunga na timu hiyo baada ya kuipiga chini ofa ya Mtibwa Sugar iliyomhitaji baada ya mkataba wake na Polisi Tanzania iliyoshuka daraja msimu kuisha na kumfanya awe huru.

Akizungumza kutoka Arusha, Afisa mtendaji mkuu wa timu hiyo, Omar Kaaya amesema wanataka kufanya Surprise (Mshangao) kwa mashabiki wao, hivyo wataweka wazi usajili wao pindi wakikamilisha.

“Kuna zaidi ya mwezi kwenye usajili, hivyo kuna mambo mengi yanaweza kujitokeza hapo, hatutaki kubahatisha ndio maana tunataka kuleta wachezaji watakaoleta tija kwenye timu yetu,” amesema.

Imefahamika kuwa mapendekezo ya benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Denis Kitambi ilikuwa ni kuletewa mshambuliaji atakayeleta ushindani mbele ya Reliants Lusajo.

Sabato alifunga mabao sita akiwa na Polisi Tanzania anaongeza nguvu msimu ujao akiungana na Erasto Nyoni (Simba SC) na Hamad Majimengi (Coastal Union).

Arsene Wenger apewa maua yake Arsenal
Nicolo Barella akoleza vita Man City, Liverpool