Afisa Mtendaji Mkuu wa Namungo FC, Omary Kaaya, amesema wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho wanawapa nguvu ya kufanya vizuri kwenye mechi watakazocheza.

Timu hiyo inayofundishwa na kocha kutoka nchini Burundi Cedric Kaze, amekiongoza kikosi hicho kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Bara msimu huu, dhidi ya JKT Tanzania amabyo walipoteza 0-1, kisha sare ya 1-1 dhidi ya KMC.

Kaaya amesema wanatambua ushindani kwenye ligi ni mkubwa, hivyo wanafanya maandalizi mazuri kupata matokeo chanya.

“Msimu mpya unakuja na ushindani wa kitofauti, wachezaji waliopo kwenye kikosi wanatupa nguvu ya kushindana na kupata matokeo mazuri kwenye mechi ambazo tutacheza.

“Kila mmoja anatambua kile ambacho tunahitaji ni matokeo mazuri na malengo yapo wazi kuonyesha ushindani kwenye mashindano ambayo tunashiriki.” amesema.

Inigo Martinez: Tutatwaa ubingwa wa Ulaya
Jurgen Klopp: Siwezi kuondoka Liverpool