Wengi walihoji uhai wa muziki wa Nandy mara baada ya Mkurugenzi na Mtayarishaji wa Vipindi Clouds Media, Ruge Mutahaba kuaga dunia ambaye ndiyo alikuwa sapoti kubwa katika muziki wa Nandy.
Nandy ameendelea kuwadhihirishia mashabiki wake kuwa kipaji anacho, nguvu anazo na kazi ya Mungu haina makosa kumchukua Ruge siyo mwisho wa muziki wake zaidi kuweka jitihada katika kipaji chake na kuleta ubora wa kazi zake.
Hayo yamedhihirishwa mara baada ya kuachia ngoma mpya aliyoimba na Willy Paul inayoenda kwa jina la Halleluyah ni moja ya ngoma kali kuliko zile za jana kuanzia Video mpaka mashairi.
Uwezo wa Nandy katika ngoma hii inadhihirisha kuwa kipaji ni kipaji tu, Nandy tayari amefunguliwa njia na Dunia ashindwe yeye kuwa anachotaka.
Hata hivyo alihojiwa na Millard Ayo namna ambavyo ataenzi maisha ya Ruge na kusema kuwa kikubwa ni kufanya kazi kwa bidii kwani Ruge alikuwa ni mchapaka kazi aliependa kuona watu wakifanya kazi.
Aidha, Kupitia ukurasa wa Mange Kimambi ameusifia wimbo huo mpya na kusema kuwa ni ”Nyimbo kali”.
Hii ni mara ya pili wawili hao kufanya colabo, ngoma yao ya kwanza ilienda kwa jina la Njiwa sasa ni Halleluyah shusha maoni yako ipi unaikubali zaidi, tuandikie hapo chini.
Itazame hapa chini.