Mwanamuziki mahiri kutoka katika tasnia ya muziki wa Bongo fleva Faustina Mfinanga Maarufu kwa jina la kisanii Nandy ametolea ufafanuzi suala la yeye na Billnass kuacha Muziki baada ya ndoa.
Dhana hiyo iliyopo kwa baadhi ya mashabiki wake kuhusu ndoa anayotarajia kufunga siku za usoni na msanii mwenzie rapa Billnas, kuwa pengine kuingia kwenye ndoa hio inaweza ikawa chanzo cha wao kupotea kimuziki kwa kuwa imekua kama utaratibu kwa baadhi ya wasanii kutosikika tena punde wanapoingia kwenye ndoa.
“Najua watu wengi fikra zao zinaona kwamba mtu flani akishaingia kwenye ndoa labda muziki ndio basi na vitu kama hivyo, ni comment ambazo naziskia mara nyingi watu wakiwa wanaziongelea. Labda niseme tu kwamba mimi ndio nitakuwa mfano wa yule mwanamuziki ambaye natokea Afrika mashariki au Afrika ambaye ameingia kwenye ndoa, tena ndoa takatifu lakini muziki wake upo pale pale namba moja so tuendelee kuombeana, mambo mazuri yanakuja, kuna maisha baada ya muziki.” Alisema Nandy
Nandy aliongeza kuwa, yeye ni binti na kuna hatua lazima azipige pamoja na kuwa msanii na ni vyema kuvitimiza hata kama ni mwanamuziki.
“So tuombeane Suala la ndoa ni la heri, lifike inshallah na maisha pia ya muziki yataedelea vile vile katika utofauti kabisa na watu wataendelea ku-enjoy.” amesema Nandy kupitia kwenye mahojiano maalum aliyofanya na mtangazaji Mammy baby kupitia kipindi cha Top20 cha Cloudsfm.
Nandy na Billnas kwa sasa wako katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa taratibu za kuelekea kufunga ndoa, ambapo mapema Februari 20, 2022 ilikuwa ni siku ambayo rapa Billnas alifanikiwa kutoa mahari kwa wazazi wa Nandy tayari kwa kung’oa jiko.