Mgombea ubunge wa jimbo la Mtama kupitia CCM, Nape Nnauye amewaahidi wananchi wa jimbo hilo kuwa endapo watampa ridhaa, atahakikisha jimbo hilo linakuwa na umeme kwenye kila kijiji.

Akiongea katika mkutano wa kampeni katika jimbo hilo jana, Nape ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, alisema kuwa anafahamu kuwa changamoto kubwa ya jimbo hilo ni ukosefu wa huduma ya umeme.

“Tukiingia madarakani, tutahakisha kuna umeme katika kila kijiji cha Mtama,” alisema Nape.

Mgombea huyo anaekabiliwa na ushindani mkali katika jimbo hilo aliwahakikishia wananchi kuwa chama chake kitashinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu huku akiwahimiza kukipigia kura chama hicho.

Lowassa Kuwakabidhi Wananchi Kiwanda Cha Mtibwa
Magufuli Kuwainua Wakulima Wa Tumbaku