Aliyewahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kutenguliwa nafasi hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, na sasa ni Mbunge wa Mtama tiketi ya CCM, Nape Nnauye leo, amekumbukia tukio lake la kutishiwa bastola wakati akitaka kuongea na waandishi wa habari katika hotel ya Protea amefunguka na kuacha ujumbe mzito.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Nape Nnauye amekikumbuka kitendo hicho kilichotokea mwaka jana 2017, siku ya Alhamisi.
“Mwaka mmoja uliopita tarehe kama ya leo Mwemyezi Mungu aliniokoa na mdomo wa bunduki wa wanyama wasiopenda haki! Mungu mkubwa, mbegu ya haki haifi!” -ameandika Nape Nnauye.
Nape katika hotuba aliyotoa siku hiyo alizungumzia juu ya haki ya waandishi wa habari, kufuatia tukio la kuvamiwa kwa kituo cha Televisheni ya Clouds, Siku ya ijumaa usiku Machi mwaka jana.
-
Serikali yapewa mwezi mmoja kulipa fidia kesi ya Babu Seya na mwanae
-
Majaliwa apongeza hatua mradi wa ujenzi uwanja wa ndege
Ambapo kama waziri wa Habari sanaa na utamaduni alilaani kutokea kwa tukio hilo na kuamua kuunda kamati ya uchunguzi kuhusiana na tukuio hilo na kuitolea ripoti kamili kupitia vyombo vya habari.
Ambapo haikumchukua muda Nape Nnauye alivuliwa kofia ya uwaziri na cheo hicho kuvalishwa Dkt. Harrison Mwakyembe, ambaye kwa sasa ndiye anayeongoza sekta ya Sanaa, Utamaduni, na Michezo akishirikiana na Naibu wake Waziri kijana, Juliana Shonza.