Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ameendelea kumshambulia mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa ambaye alikuwa kada mkongwe wa chama hicho.

Nape ambaye amekuwa akitumia mifano mbalimbali kumchafua Lowassa iwemo kumfananisha na oil chafu iliyokuwa kwenye injini ya chama hicho, jana ameibuka kivingine na kumdhihaki kuwa anaujua ‘msuli’ wake na ameshindwa kufurukuta kwake kwa takribani miaka 12 ya uadui wao.

Kada huyo wa CCM ambaye anaonekana kutafuta kila namna ya kuivuruga nguvu kubwa ya Edward Lowassa iliyoonekana hivi karibuni kwa wananchi, alisema kuwa anamfahamu vizuri mgombea huyo wa Chadema na kwamba ‘hafai hata kuwa balozi wa nyumba kumi’.

“Mimi sijaanza vita jana, nimeanza nae miaka 12 iliyopita naye anajua huu msuli wangu mkubwa sana. Maana najua hafai, hafai hata kuwa balozi wa nyumba kumi,” alisema Nape.

Enzi za urafiki wa mashaka

Enzi za urafiki wa mashaka kati ya Nape na Lowassa 

Nape aliwashambulia pia Ukawa na kudai kuwa wanatumia vipande vya hotuba ya Mwalimu Julius Nyerere huku wakiacha vipande ambavyo vingeonesha wazi kuwa havikubaliani nao.

CCM tayari wameweka wazi timu ya watu 32 ambao watazunguka kumnadi mgombea wao wa urais, Dk. John Magufuli huku Chadema na Ukawa kwa ujumla wakisubiriwa kuiweka wazi timu yao.

Hata hivyo, mikutano mitatu ya hivi karibuni ya Edward Lowassa imeonesha kuwa tishio kwa wapinzani wake kutokana na kuvuta umati wa watu ambao haujawahi kushuhudiwa.

 

TFF Yavunja Ukimwa, Yaanika Ratiba Ya 2015-16
FIFA Kukutana Na Marafiki Wa Kibiashara