Mbunge wa Jimbo la Mtama kupitia chama cha mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amependekeza kuongezwa kwa wigo wa walipa kodi, ili kuwaondolea mzigo baadhi ya watumishi na wafanyakazi katika sekta mbalimbali nchini.

Ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akizungumza juu ya mgawanyo wa fedha hususani kwenye sekta ya Kilimo, ambayo imeonekana ikiongoza kwenye uchangiaji wa pato la taifa.

Amesema kuwa wigo wa walipa kodi kwa muda sasa kuna takwimu kwamba walipa kodi milioni 14 wanalipa milioni 2.4, ambapo mzigo wa wawalipa kodi wengi unabebwa na walipa kodi wachache.

”Wigo wa walipa kodi kwa muda sasa kuna takwimu kwamba walipa kodi milioni 14 wanaolipa milioni 2.4, mzigo wa walipa kodi wengi unabebwa na walipa kodi wachache, nadhani huu wigo tungeanza nao kidogo kidogo ili tuweze kupunguza kodi kwa wafanyakazi,” amesema Nape.

Kwa sasa Bunge linaendelea jijini Dodoma ambapo Wabunge wanajadili Bajeti ya mwaka 2019/2020 ambayo iliwasilishwa na Waziri wa Fedha Alhamisi ya wiki iliyopita.

Simba yadondosha kifaa kingine
Ujangili wapungua kwa 70%, Waziri aeleza sababu