Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amekanusha taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai wizara yake imepiga marufuku kuvaa vimini na mlegezo kuanzia Januari Mosi mwakani.

Nape ameeleza kuwa taarifa hizo ni za uongo na upotoshaji kwa kuwa hakuna taarifa ya aina hiyo iliyotolewa na wizara yake. Hivyo, amevitaka vyombo vinavyohusika kuchukua hatua dhidi ya watu waliohusika kufanya upotoshaji huo.

“Hizo taarifa ni uzushi mtupu na uongo, mamlaka husika wachukue hatua, watimize wajibu wao, watumie sheria iliyopo kuwachukulia hatua,” Nape ananukuliwa.

Wanaume 1500 wajitangaza Kuwa Mashoga Mkoani Iringa, Wanafunzi waongoza
Mke wa T.B Joshua aeleza jinsi alivyoanza Mapenzi na Mumewe, Aulizwa alivyo 'Kitandani'!