Baada ya kimya cha muda mrefu, hatimaye Chama Cha Mapinduzi Tanzania kimezungumzia uamuzi wa waziri wa zamani, Edward Lowassa na wanachama wengine wa chama hicho kuhamia kambi ya upinzani.

Akiongea na waandishi wa habari jana, Nape ametumia mifano mbalimbali ya kejeli katika kuhalisha mtazamo wake kuwa waliokihama chama hicho walikuwa hawafai kuendelea kuwepo.

Alisema kuwa kitendo cha watu hao kuhama kinaipa unafuu CCM kwa kuwa ni kama mtu anaebadilisha oil chafu kwenye injini yake ili kuiokoa, “uking’ang’ana na oil chafu injini yako itanoki.”

Pia, Nape alidai kuwa kuondoka kwa wanasiasa hao kwenye chama hicho kwa sababu hawakutimiziwa kile walichotaka na kujiabisha kwa kujivua nguo mbele ya wananchi.

“Kwamba CCM ilikuwa njema kwa miaka yote ambapo wewe ulikuwa na fursa, ikifika mahali unaambiwa wewe hauna fursa kwa jambo unalolitaka moja basi unaona CCM haifai kwa kila kitu. Bila shaka wamejivua nguo mbele za watu na watanzania watawaadhibu,” alisema Nape.

Hata hivyo, Nape alisisitiza kuwa ni kawaida katika siasa watu kuhama chama kimoja kimoja kwenda chama kingine na kwamba wapo ambao wataendelea kuhama kutoka CCM kuingia upinzani na wapo watakaotoka upinzani kurudi CCM.

Nape aliweka mkazo kuwa pamoja na mambo mengine yote, CCM lazima itaibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.

 

Dk. Slaa Kuiokoa Chadema Dhidi Ya Mtego Wa CCM?
Magufuli Kufunga Barabara Za Dar Leo