Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye ametoa kauli zake tatu ambapo katika kauli ya kwanza alikuwa amelenga kuwapa ujasiri vijana na Watanzania kiujumla kuchukua hatua katika mambo fulani.

Ameyaadika hayo kupitia  ukurasa wake wa twitter na kuwambia kuwa unapoona umekosa matumaini juu ya jambo fulani hupaswi kusita kufanya maamuzi huku ukimuamini Mungu kwani yeye hutoa njia.

“Mwenyezi Mungu hufanya njia pasipokuwa na njia! Amini na chukua hatua,”ameandika Nape katika ukurasa wake wa twitter

Aidha Mbunge huyo amezidi kuwasisitiza Watanzania na kuwataka kuwa na busara katika mambo yao hata mambo yanapokwenda ndivyo sivyo amewataka kutumia busara zaidi kuweza kuyatatua.

Hata hivyo, Mbunge huyo wa Jimbo la Mtama siku za hivi karibuni amekuwa akitoa kauli tofauti tofauti huku Watanzania wengi wakishindwa kuzielewa.

Video: Sitaki kuzozana na familia ya Lissu - IGP Sirro, Angellah Kairuki atikisa kila kona
Masauni aagiza kushugulikiwa kwa mkandarasi