Mbunge wa Jimbo Mtama kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amewataka Wabunge wa Tanzania bila ya kujali itikadi ya vyama vyao kuwa kitu kimoja na kumuunga mkono Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe juu ya hoja yake binafsi aliyoiwasilisha kwa Katibu wa Bunge.
Nape ametoa kauli hiyo mara baada ya kuibuka kwa baadhi ya wabunge wa upinzani kumpinga Bashe na kumuita mnafiki kwa anachotarajia kukifanya.
“Kazi ya Mbunge ni pamoja na kuwasemea wananchi ambao kwa namna moja ama nyingine hawana fursa ya kwenda wenyewe Bungeni. Tumuunge mkono Mhe. Bashe bila kujali tofauti zetu za itikadi, dini au rangi,”amsema Nape
Hata hivyo, Nape amedai hoja binafsi ndani ya Bunge ni moja ya njia za kutafuta ukweli na suluhisho juu ya jambo fulani ambalo linatafutiwa ufumbuzi wake.