Mbunge wa Jimbo la Mtama (CCM) Nape Nnauye amesema kuwa tetesi zilizokuwa zikizagaa na kuzungumzwa kuwa naye yuko mbioni kuhama chama chake cha mapinduzi kama ambavyo amefanya Lazaro Nyalandu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost picha ambayo wako watatu akiwemo yeye, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, na aliyekuwa Mbunge kupitia CCM ambaye amejivua uanachama, Lazaro Nyalandu

Aidha, Nnauye ameandika maneno ambayo yanaonyesha hana mpango wa kuhama chama chake kama ambavyo inahisiwa na watu mbali mbali, lakini akasema atainyoosha CCM akiwa ndani ya chama hicho.

“Chama cha siasa ni itikadi, itikadi ni imani. Siamini sana katika kubadili imani kienyeji. Nitashughulikia mapungufu nikiwa ndani na sio nje ili kukiweka sawa chama kinapoyumba na si vingine,” ameandika Nape

Hata hivyo, Kufuatia kuonyesha msimamo huo, hatua hii moja kwa moja itafunga majadiliano ya watu katika sehemu tofauti kuwa ana mpango wa kukitosa Chama cha Mapinduzi c CCM.

Simba SC waifuata Mbeya City kwa usafiri wa anga
Nyalandu: Kuhama CCM nimefuata ushauri wa Baba wa Taifa