Katika kuhakikisha wananchi wanamuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli, kupiga vita madawa ya kulevya, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye amevishauri vyombo vya habari nchini kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili ujumbe uwafikie haraka zaidi wananchi kuhusu vita hiyo dhidi ya madawa ya kulevya nchini.
Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliofanyika katika Chuo Kikuu huria cha Tanzania na kusisitiza kuwa vyombo vya habari viwe sehemu ya kuwaunganisha watanzania katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.
“Wanahabari tuliunganishe taifa letu tuwe kitu kimoja katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya” amesema Nnauye.
Ameongeza kuwa sasa ni wakati wa watu wote kuungana kwa pamoja zikiwemo tasnia zilizopo katika Wizara yake ikiwemo tasnia ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwani vita hii ni ya watanzania wote na sio mtu mmoja au Serikali pekee.
Aidha. Nape amevitaka vyombo vya habari kutobaki nyuma katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya na kuhakikisha haki inatendeka na vita dhidi ya madawa ya kulevya vinashinda