Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya, NASA umetaka nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Teknolojia ya Mawasiliano wa Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi (IEBC) apewe mtaalam kutoka nje ya nchi hiyo.
Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za muungano mkuu wa upinzani – NASA, kiongozi wa chama cha Amani, Musalia Mudavadi, na Wakili James Orengo, wamesema wanataka nafasi ya Marehemu Msando itolewe kwa raia wa Marekani ama Uingereza.
Aidha, wamechukua hatua hiyo, mara baada ya Serikali kukaa kimya bila kutoa tamko lolote kuhusu kifo cha Msando ambaye alikuwa mhimili mkubwa katika masuala ya teknolojia kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 8 mwaka huu.
Kwa upande wake, shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limezitaka mamlaka nchini Kenya kuchunguza mauaji ya Christopher Msando. ambapo limesema kuwa mauaji hayo ni pigo kwa uchaguzi mkuu ujao nchini humo.
-
Museveni asema yuko fiti, ‘sijaugua kwa miaka 31’
-
Video: Sumaye afunguka mazito kuhusu Wema Sepetu
-
Taasisi za umma zabanwa kuhusu matumizi ya kuni
Hata hivyo, Balozi wa Marekani nchini Kenya, Robert Godec, na mwenzake wa Uingereza, Nic Hailey, wamesema kuwa wamesikitishwa na mauaji ya Msando ambayo yametokea siku sita kabla ya uchguzi mkuu kufanyika.