Mtaalamu wa Elimu ya nyota, kutoka kituo cha NASA cha Marshall Space Flight Center cha nchini Marekani, Adam Kobelski amesema Jupiter, itakuwa karibu zaidi na Dunia baada ya takriban miaka sitini na kutoa fursa ya kuiona Sayari hiyo kubwa katika mfumo wa jua, kabla na baada ya Septemba 26.
Kobelski, ameyasema hayo hii leo Septemba 26, 2022 nchini Marekani na kuongeza kuwa miezi minne mikubwa zaidi inayozunguka sayari ya Ganymede, Europa, Io na Callisto pia itaonekana, wakati Jupiter ikiwa umbali wa ndani ya kilomita milioni 590 na kusisitiza wote walio katika eneo la hali ya hewa nzuri, kutumia nafasi hiyo kutazama.
Jupiter, inajulikana kwa wanadamu kama Sayari yenye mwanga mkali angani tangu zamani, lakini Galileo Galilei, alikuwa wa kwanza kutazama sayari hii kubwa kwa kutumia darubini ya mapema mwaka 1610.
Karne nne baadaye, lenzi kubwa na bora zaidi, pamoja na vyombo vya anga kama Voyagers na Juno, vilifanya uchunguzi wa mara kwa mara wa sayari na hivi majuzi, chombo cha anga la juu cha DART, kilijiunga na orodha ya mashine zilizoinasa Jupiter na kutuma picha zake Duniani kabla ya kugongana na asteroid iliyo karibu.
Jupiter itakuwa ‘katika upinzani’ kwa Jua na Dunia, ikimaanisha kuwa jua linapotua upande wa magharibi, Jupita itakuwa ikichomoza upande wa mashariki na kwa wale wanaotazama kwa macho, wataona Sayari ya Jupita na miezi yake ikionekana kama taa angavu angani.
NASA inasema, darubini ya kuakisi ya inchi nne itatosha kunasa tukio la Jupita, lakini bado watu wanaweza kuona nukta iliyofifia, nyekundu-machungwa, kulingana na ubora wa darubini, anga na hali ya hewa.