Kocha Mkuu wa Young Africans, Nasreddine Nabi amejikuta akipatwa na kigugumizi juu ya timu anayotamani kukutana nayo kama atafuzu katika hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Young Africans kwa sasa wapo katika hatua ya Robo Fainali huku mchezo wao wa Mkondo wa Kwanza wakiwa wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Rivers United ugenini, jambo ambalo ni faida kwao.

Kocha Nabi amesema kuwa: “Sisi binafsi kama Young Africans bado hatujafuzu kwenda katika hatua ya Nusu Fainali, bado tuna mtihani mbele ya Rivers tukiwa kwetu, kwa wale amabo wanaona kuwa kazi tumemaliza wanatakiwa kutambua huu ni mpira wa miguu.”

“Tunakwenda kuweka mipango yetu kwaajili ya kupata matokeo mazuri katika mchezo wetu wa marudiano, kuhusu nusu fainali siwezi kusema nawataka Marumo wala Pyramid mpaka pale ambapo tutakamilisha ratiba yetu,” amesema kocha huyo.

Young Africans itakuwa mwenyeji wa Rivers United katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam siku ya Jumapili (April 30) huku ikihitaji ushindi wowote au sare ili kujihakikishia nafasi ya kutinga Nusu Fainali.

Kwa Upande wa Rivers United Itatakiwa kushinda mabao 3-0 au zaidi ili kusonga mbele.

Mshindi wa jumla wa mchezo huo atakutana na mshindi kati ya Pyramids na Marumo Gallants kwenye Hatua ya Nusu Fainali.

Mtoto Mustapha afika Ikulu kumshukuru Rais Samia
Nape ataka mipango endelevu ya Vyombo vya Habari