Kocha Mkuu wa Young Africans Nasreddine Nabi amesema wakati wanajiandaa kuelekea nchini Sudan tayari kwa mchezo wa Mkondo wa Pili wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Al Hilal, ana uhakika Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo hawataamini kitakachotokea ugenini.

Young Afriocans itacheza mchezo huo mjini Khartoum-Sudan Jumapili (Oktoba 16) katika Uwanja wa Al Hilal, huku ikiwa na deni la kupindua matokeo ya sare ya 1-1 yaliyopatikana Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma lililopita (Oktoba 08).

Nabi amesema wanafahamu makosa waliyoyafanya katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza, lakini amesisitiza watakachoenda kukifanya ugenini jijini Khartoum, wengi hawataamini.

Amesema hawataenda Sudan kinyonge kwani bado wana dakika 90 za kuamua matokeo yatakayowapeleka hatua ya makundi ama kuangukia kwenye play-off ya Kombe la Shirikisho Afrika.

“Kuna sehemu tulifanya makosa sana ya kutotumia nafasi ambazo tulizitengeneza, tulicheza vizuri sana kipindi cha kwanza hasa dakika 55 za kwanza, tuliporuhusu goli hatukuonyesha ukomavu, tulinyon g’onyea sana,” amesema Kocha Nabi

“Tunajua makosa yetu pia tunafahamu mashabiki wetu wameumia sana, huu ndio mchezo wa soka, hatujakata tamaa na wala hatutakwenda kurudiana nao tukiwa na akili ya kujilinda. Tutakwenda kuipigania Yanga, hii ni vita ya soka bado haijaisha tutazungumza na wachezaji kubadilisha muelekeo wa akili yao.”

Simba SC yatoa tahadhari Kimataifa, Ligi Kuu
Kocha Nabi abadilisha DOZI Young Africans