Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi (NATO), umelazimika kuitisha kikao cha dharura kujadili hali ya usalama wa nchi za ukanda huo baada ya Uturuki kushambulia ngome ya dola ya kiislamu (IS) nchini Syria na PKK nchini Iraq.

Waziri Mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoglu aliviambia vyombo vya habari kuwa uamuzi wa Uturuki kushambulia ngome za IS nchini Syria uliozua mashambulizi mengine dhidi ya kundi la Ki-Kurdish (PKK) unaweza kubadili kabisa ‘mchezo wa vita’ katika ukanda huo.

Jumapili, Uturuki ilituma vikosi vyake vya anga kufanya mashambulizi dhidi ya kundi la PKK kaskazini mwa Iraq huku mashambulizi ya Syria yakitajwa kulenga kuvisaidia vikosi vinavyopambana na IS nchini Syria.

“Uwepo wa Uturuki ambayo itatumia ipasavyo vikosi vyake itapelekea matokeo ambayo yatabadili kabisa mchezo nchini Syria, Iran na ukanda mzima na kila mmoja anapaswa kuliona hilo,” alisema Davutoglu.
Hata hivyo, waziri mkuu huyo alisisitiza kuwa Uturuki haitapeleka vikosi vya ardhini kupambana na makundi hayo ya kigaidi.

Kufuatia hali hiyo, Uturuki imeomba NATO kuitisha kikao cha dharura ambacho kitafanyika kesho kujadili muenendo wa mashambulizi hayo na madhara makubwa yanayotarajiwa.

Uturuki imepanga kuishawishi NATO kuungana rasmi katika mashambulizi ya kijeshi dhidi ya makundi ya kigaidi katika ukanda huo.
Nchi zote za Magharibi zenye nguvu kubwa zilizopeleka vikosi vyake kupambana na IS zimesita kupeleka vikosi vya ardhini. Wachambuzi wa masuala ya kivita wanaeleza kuwa ni vigumu kulimaliza kundi la IS bila kutumia vikosi vya ardhini.

‘Wanasiasa Hawa…WOTE MANZI GA NYANZA’
Zitto Kabwe: ACT Ina Miiko Ya Maadili Tofauti Na Ukawa