Mkosoaji wa rais wa Urusi Vladimir Putin, Alexei Navalny amekamatwa baada ya kurejea mjini Moscow kwa ndege akitokea Ujerumani, miezi mitano baada ya kushambuliwa kwa sumu ya neva ambayo nusura imuue.

Mwanaharakati huyo, mwenye umri wa miaka 44, alichukuliwa na polisi katika kitengo cha udhibiti wa pasipoti katika uwanja wa ndege wa Sheremetyevo.

Maelfu ya watu walikuwa wamekusanyika katika viwanja tofauti vya ndege vya mjini Moscow kuipokea ndege yake iliyokuwa ikitokea mjini Berlin, lakini ndege yake ilielekezwa kwenye uwanja tofauti.

Navalny anazilaumu mamlaka za Urusi kwa jaribio la kumuua mwaka jana ambalo Utawala wa Kremlin unakana kuhusika nalo licha ya kwamba madai ya mwanasiasa huyo wa upinzani  yamekua yakiungwa mkono na ripoti za waandishi wa habari wa taarifa za uchunguzi.

Navalny alipewa sumu mwezi Agosti mwaka jana na kuzimia katika safari ya ndege ya kimataifa, ambapo alisafirishwa hadi nchini Ujerumani kwa ajili ya kupata huduma za matibabu za dharura.

Ulinzi waimarishwa Marekani
Nyama ya kitimoto yapigwa marufuku