Rapa kutoka Uganda, Navio ametangaza ujio mpya wa kundi lake la ‘Klear Kut’ linaloundwa na Papito, Abba Lang, JB na Mith, baada ya muda mrefu wa kufanya kazi kama Solo.

Navio ambaye amejiunga na wasanii wakubwa wa Afrika jijini Nairobi kurekodi msimu mpya wa Coke Studio Afrika, amewaambia waandishi wa habari kuwa wamejipanga kulipua tena anga na muziki mzuri kwa kuachia album yao ya pamoja.

“Klear Kut ni kundi kongwe na bado ni moja kati ya makundi bora zaidi Afrika Mashariki. Tumefanya mikono mingi Uganda, ndio sababu tukatengeneza jina kubwa. Tunatarajia kuwa na ujio mzuri na album inatoka mwaka huu 2015 na wimbo mpya ‘Let it rain’ utaachiwa ndani ya miezi miwili,” Navio alifunguka.

Klear Kut lilianzishwa Agosti 2000 na kupata nafasi ya kukubalika zaidi nchini Uganda na Kenya.

Dada Wa Lupita Nyong’o Akerwa Na Swali La Mhudumu Wa Hotel kuhusu Lupita
CCM Kushitakiwa Kwa Kuanza Kampeni Mapema