Navy Kenzo ni kundi ambalo linaundwa na wasanii wawili ambao wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi tangu kuanzishwa kwa kundi hilo na wamejaliwa mtoto mmoja.

Aika na Nahrel wiki iliyopita ya septemba 27 walifanikiwa kuachia ngoma yao mpya inayojulikana kwa jina la “Katika” ambao wamemshirikisha C.E.O wa WCB Wasafi Diamond Platnumz.

Kundi hilo lilikuwa kimya kwa muda kidogo ni baada ya Aika kupata ujauzito na kufanikiwa kujifungua salama mtoto wa kiume na  wamerudi rasmi kwenye muziki baada ya kutoa ngoma hiyo inayoendelea kufanya vizuri kwa sasa kwa kupata viwers  wengi zaidi kwa muda mfupi huku wakiahidi kuachia ngoma nyingine kali.

Mara baada ya wasanii hao kuachia  nyimbo hiyo ya ”Katika” kumekuwa na tetesi kuwa huenda kundi hilo  limesainiwa na lebo kubwa hapa nchi WCB lakini baada ya wasnii hao  kuulizwa swali wamekanusha uvumi huo uliovumishwa na moja ya wasanii toka kundi la Wasafi.

Navy Kenzo wamesema si kweli wamejiunga na Wasafi na kuongezea kwamba wapo chini ya meneja wao na si kundi la wasafi kama ilivyovuma hapo awali.

Moja kati ya wasanii wa WCB Harmonize  aliandika katika mtandao wake wa kijamii kuwa “Navy Kenzo karibuni Usafini” na kudai kuwa yeye hapendi vitu vya siri kwani hawamuogopi mtu yeyote lakini baada ya Harmonize kumaliza maneno hayo Nahrel alijibu na kuonyesha kuiunga mkoo kauli hiyo ya Harmonize.

Ali Kiba aamsha na ujio wa ngoma mpya 'Hela'
Zaidi ya Milioni 400 zapatikana Simba SC Vs Young Africans