Rais Dkt John Magufuli ametoa siku 7 kwa wafanyabiashara bingwa wa kukwepa kodi kuhakikisha wanajisalimisha wao wenyewe kwa kulipa hela za serikali.

Ametoa amri hiyo Alhamis hii alipokutana na wafanyabiashara mbalimbali ikulu jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imekuja siku chache baada ya Magufuli na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa kuitikisa bandari ya Dar na mamlaka ya mapato, TRA.

Kasi yake ilisababisha kuota kibarua cha aliyekuwa kamishna mkuu wa TRA Rished Bade pamoja na maafisa wengine wanaohisiwa kushiriki kwenye tukio la upotevu wa makontena zaidi ya 300 kwenye bandari hiyo.

Waziri Mkuu Ashtukiza Tena Bandarini, Akuta Madudu Mengine
Mwanamuziki mkongwe Kasongo Mpinda aaga dunia