Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanzia, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, Kamishna Mkuu wa TRA, Dkt. Edwin Mhede pamoja na Katibu Tawala wa mkoa wa Njombe, Charles Kichere kufanya kazi kwa bidii na kutatua changamoto na kero mbalimbali zinazo wakumba wafanyabiashara, wawekezaji pamoja na wananchi.

Ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es salaam mara baada ya kuwaapisha viongozi hao, ambapo amesema kuwa kuna changamoto mbalimbali zinazo wakabiri wafanyabiasha na wawekezaji nchini.

Rais Magufuli amewaapisha waziri wa biashara na viwanda, Innocent Bashungwa akichukua nafasi ya Joseph Kakunda, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dkt. Edwin Mhede akichukua nafasi ya Charles Kichere ambaye naye pia ameapishwa kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Njombe

”Mimi nadhani hao badala ya kuwapongeza, wangewapa pole, maana mimi nachotaka ni kazi tu, na kama hautaweza kutatua changamoto hizo zinazo wakabiri wawekezaji na wafanyabiashara wewe nitakutumbua tu kwani waliokutangulia ni wangapi,”amesema Rais Magufuli

Aidha, Rais Magufuli amemtaka waziri Bashungwa kutafuta wawekezaji nje ya nchi ili kuja kuwekeza katika viwanda vya Korosho mkoani Mtwara na vingine vilivyotelekezwa hapa nchini ili Watanzania wengi waweze kuajiriwa.

Pia amesema kuwa kuna fursa nyingi za uwekezaji hapa nchini lakini viongozi wengi wamekuwa hawana ukaribu na wafanyabiashara ambao ndio wadau wakuu wa kukuza uchumi, akitolea mfano kwa aliyekuwa waziri wa viwanda na biashara, Joseph Kakunda ambaye hata wafanyabiashara na wawekezaji walikuwa hawamfahamu.

 

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 11, 2019
Faida 7 za kula tango