Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) leo August 15, 2016 limetangaza kumfungulia msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego kufanya kazi yake ya muziki akiwa kwenye uangalizi maalum katika kuhakikisha anaendelea na shughuli za sanaa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.

Hii ni kufuatia tamko la BASATA la tarehe 27, 7, 2016  la kumfungia msanii huyo wa Bongo Fleva kutojihusisha na kazi ya sanaa kwa muda usijulikana.

Akitoa tamko hilo la kumfungulia Nay wa Mitego, Katibu mkuu wa BASATA Godfrey L. Mngereza amesema msanii huyo ametekeleza adhabu zote ambazo ni:-

  • Kulipa faini ya Shilingi milioni moja (1,000,000/-)
  • Kuomba radhi watanzania kupitia mkutano wa waandishi wa habari na kwenye akaunti  zake za mitandao ya kijamii
  • Kuhakikisha amesajiliwa na kuwa na kibali cha kuendesha shughuli za Sanaa
  • Kuufanyia marekebisho wimbo wake wa ‘Pale Kati’ ili ubebe maudhui yenye maadili

Mngereza pia amesema kuwa BASATA inaendelea kuufungia wimbo wa ‘Pale Kati’ hadi hapo litakapojiridhisha umekidhi vigezo vya kimaadili pamoja na kwamba msanii huyo amepeleka marekebisho mara mbili ya wimbo huo hivyo kumtaka Nay wa Mitego kuendelea kuufanyia marekebisho wimbo wake huo kama bado anauhitaji.

Mrema awatofautisha Dk. Mashinji na Dk. Slaa
Alexandre Lacazette Atuma Salamu, Apiga Tatu Dhidi Ya Nancy