Kiungo Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain Neymar, Neymar da Silva Santos Júnior ametozwa faini ya Dola milioni 3.33 na mamlaka ya nchini Brazil kwa kukiuka kanuni za mazingira za eneo la Pwani ambapo amejenga jumba lake la kifahari katika Jiji la Mangaratiba nje ya Rio de Janeiro.

Mamlaka ya Jiji la Mangaratiba imesema katika taarifa yake kuwa imetoa faini nne baada ya Neymar kushtakiwa kwa kujenga ziwa bandia katika jumba lake la kifa hari kinyume cha sheria.

Hata hivyo, wasemaji wa Neymar mwenye umri wa miaka 31, walikataa kutoa maoni yoyote kwa vyombo vya habari.

Neymar anaweza kukata rufani dhidi ya uamuzi huo, ambao utakabidhiwa kwa polisi kwa uwezekano wa kufunguliwa mashtaka.

Juni 22, maofisa wa mazingira walikagua nyumba ya Neymar baada ya malalamiko yaliyotolewa, ambayo yalionesha kazi kubwa ya ujenzi iliyofanywa bila idhini ya mazingira.

Mamlaka ya Jiji la Mangaratiba imesema katika taarifa yake kwamba makosa kadhaa ya mazingira yalifanywa “katika ujenzi wa ziwa bandia kwenye jumba hilo.”

Miongoni mwa ukiukwaji huo ni pamoja na kuzuia na kuchepusha maji ya mto bila kibali, kusogezwa kwa ardhi na kukandamiza mimea bila idhini.

“Idara ya Mazingira, pamoja na kutumia faini hizo kwa kuzingatia uharibifu wa mazingira uliotokea, imetoa taarifa kwa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka, Polisi, Polisi wa Ulinzi wa Mazingira na Vituo vingine vya udhibiti wa mazingira,” imeeleza taarifa hiyo.

Kampuni iliyojenga ziwa hilo la bandia, Genesis Ecossistemas, ilisherehekea kazi hiyo kwenye chaneli zake za mitandao ya kijamii. Ilisema ziwa hilo lina ukubwa wa mita za mraba 1,000.

Usajili wa Azam FC washangaza
TPLB yazikumbusha klabu kutii kanuni