Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inafanya kazi na ofisi ya mazingira ya umoja wa mataifa katika kufanya majaribio ya rasimu ya methodolojia ya kupima kiashiria namba 17.14.1 cha malengo ya maendeleo endelevu, (SDGs) ambacho kinafuatilia idadi  ya nchi zenye mifumo ya kuimarisha mahusiano ya kisera kwa ajili ya mpango wa maendelelo endelevu.

Hayo yamesemwa na Dkt Albina Chuwa Mtakwimu mkuu wa Serikali wakati wa ufunguzi wa warsha ya majaribio ya rasimu ya metghodolojia.

Amesema kuwa kutokana na sheria ya Takwimu a mwaka 2015 na marekebisho yake ya 2018 na 2019 imepewa jukumu la kutoa na kuratibu utoaji na usambazaji wa takwimu rasmi.

”kama mnavyofahamu lengo namba 17 la SDGs linazungumzia ushirikiano na njia za utekelezaji wa malengo ya SDGs ili kufikia malengo yaliyotarajiwa” amesema Chuwa.

Amesema kuwa hali hii itawezesha kufikia malengo ya jumla ya SDGs katika nyanja zake tatu kiuchumi , kijamii na kimazingira kwa usawa na kupunguza atahari zinazoweza kutokesa kutokana na mgongano wa kisera na pia kusaidia kutoa sera ambazo kwa pamoja zina mwelekeo sawa.

Hatahivyo amesema tangu kupitishwa kwa Agenda ya malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Asasi zisizo za kiserikali na washiriki wa maendeleo imejidhatiti katika utekelezaji , ufuatiliaji na tathimini ya malengo hayo.

Luc Eymael mambo safi Young Africans
Ufilipino: Hofu yazidi mlipuko wa Volcano