Afarah Suleiman – Arusha.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu – NBS, imetoa mafunzo ya siku mbili kwa Waandishi wa Habari wa Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara, yanayolenga usambazaji na matumizi ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022,.
Katika Semina hiyo iliyofanyika jijini Arusha, Kamisaa wa Sensa Tanzania, Anna makinda amewataka Wanahabari kuyatumia vizuri mafunzo hayo katika kupeleka uelewa kwa Wananchi, juu ya maswali ya Sensa ya watu na makazi pamoja na matumizi ya matokeo hayo ya Sensa.
Amesema, Wanahabari wanatakiwa kufanya kazi kwa uhuru na kujiamini wanapokuwa katika majukumu yao, kwani wao ni nguzo muhimu katika kuiunganisha Serikali na Wananchi hasa kwenye kuibua na kutatua changamoto mbalimbali, hivyo watumie Takwimu sahihi na kuleta matoeo.