Chama cha NCCR-Mageuzi kupitia wajumbe wake kimemteua Yeremia Kulwa Maganja kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi utakaofanyika Tarehe 28 Oktoba 2020.

Mkutano huo umefanyika Agosti 7, 2020 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Slaam na kuongozwa na mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia.

Akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi Anthony Komu amesema wajumbe waliopiga kura ni 258, kura saba zimeharibika, kura 20 zilipigwa hapana na kura 231 zimepigwa ndiyo na kupelekea Maganja kushinda kwa aslimia 89.

Ikumbukwe Maganja aliyejiunga na NCCR mageuzi akitokea ACT Wazalendo alikokuwa mwenyekiti wa chama hicho amepewa fursa kwa mujibu wa katiba yao kumtangaza mgombea mwenza ambaye ni Haji Ambari Khamisi

Hata hivyo mgombea huyo aliyechukua fomu ya kuwania Urais, Zanzibar ameahirisha kuwania nafasi hiyo ndani ya mkutano na kusema umri umekwenda.

Aidha msimamizi wa uchaguzi Komu amesema kutokana na Zanzibar kutokuwa na mgombea wa Urais kupitia tiketi ya NCCR Mageuzi Maganja ataona vyama ambavyo watashirikiana katika nafasi ya Urais.

Lissu kuchukua fomu ya urais leo
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 8, 2020