Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema kuwa Jeshi la Polisi halipaswi kumkamata mtu asiyehusika na kosa kwa niaba ya mtuhumiwa.
Ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum (Chadema), Devotha Minja alipotaka kujua kuhusu polisi kumkamata mbadala wa mtuhumiwa pindi wanapomkosa muhusika.
Nchemba amesema kuwa Jeshi la Polisi linafanyakazi kwa mujibu wa sheria, hivyo hakuna mtu anayeruhusiwa kuadhibiwa kwa niaba ya mwingine.
“Kosa linabaki kwa muhusika na kama kuna mtu anaweza kusaidia afanye hivyo, lakini si kuchukua hatua kwa mtu mwingine kuwa mbadala wake,”amesema Dkt. Nchemba