Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini Mwigulu Nchemba ametoa onyo kali kwa watanzania wasiokuwa na kitambulisho cha Taifa na kusema kuwa mchakato huu ukiisha mtu akiwa hana kitambulisho hatotambulika kama ni Raia wa Tanzania.

‘’ Baada ya mchakato huu kuisha tukamkuta mtu hana kitambulisho maelezo yake yatakuwa ni magumu kueleweka kama kweli yeye ni mtanzania halali” amesema Nchemba.

Aidha ameagiza kila mtanzania kujiandikisha ili kupata kitambulisho cha taifa kwani sio ombi bali ni lazima kwa kila mtanzania kutambuliwa kwa kitambulisho hicho.

“Hili zoezi la vitambulisho vya utaifa ni lalazima kwa kila mtanzania aliye nchini, ni kosa kubwa kama wewe ni raia ukaamua kukaidi ikiwa Rais wetu Magufuli ameamua kutoa vitambulisho hivyo bure bila malipo yoyote”–Dr Nchemba

Nchemba amezungumza hayo pindi akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Ruvuma

 

Mkaguzi ajinyonga kwa kipande cha chandarua
Kauli ya Kakobe yamtia mikononi mwa TRA