Ameyasema hayo wakati akizungumza na madareva wa bodaboda Mkoani Shinyanga ambao wanapatiwa mafunzo ya usalama barabarani ambapo amewataka polisi wakiwakamata madereva hao wakiwa hawana kofia ngumu kuwaweka ndani.
Amesema kuwa kama abiria akikataa kuvaa kofia ngumu wakati pikipiki ina kofia hizo basi naye akamatwe na dereva pikipiki achiwe aendelee na biashara kwani kila mtu lazima atimize wajibu wake.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Steven Masele amesema kuwa zamani palikuwa na msuguano mkubwa sana kati ya madereva wa pikipiki na askari polisi hali iliyopelekea kutokuwa na mahusiano mazuri kati yao.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoani wa Shinyanga, ACP Simon Haule amesema mafunzo hayo ni utekelezaji wa maagizo na Mkuu wa Mkoa baada ya wananchi wengi kutojua au kutokutumia sheria ya matumizi ya barabara hasa katika mzunguko ( roundabout).